Saturday, May 18, 2013

DR.SLAA ANAANZA ZIARA YA UJENZI WA CHADEMA MKOA WA MANYARA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbroad Slaa, anatarajiwa kuanza ziara ya ujenzi na kukagua uhai wa chama katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Mkoa wa Manyara, siku ya Jumamosi, tarehe 18-26, Mei 2013
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt. Slaa ataambatana na watendaji wa Makao Makuu ya CHADEMA pamoja na wabunge wote wa CHADEMA Mkoa wa Manyara.
Akiwa katika ziara hiyo, mbali ya kupokea taarifa na kukagua uhai na ujenzi wa chama katika maeneo atakayopita, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara takriban miwili kwa kila siku pamoja na mikutano ya kikazi ya ndani, ambapo atakutana na wanachama na viongozi wa maeneo husika.
Ratiba ya ziara hiyo itakuwa kama ifuatavyo;
 Atawasili Babati Mjini 18/5/2013 asubuhi; ambapo kutakuwa na mapokezi na kisha salamu kwa wananchi eneo la Minjingu, baadae atakuwa na mkutano wa hadhara saa 9 mchana viwanja vya Kwaraa, Babati mjini.

Akiwa njiani kuelekea Hanang, tarehe 19/5/2013, Katibu Mkuu atapita na kuwasalimia wananchi wa maeneo ya vijiji vya Masqaloda, Measkron, Nangwa na Dirma, kabla ya kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Balangida na Gendabi (Hanang).


Tarehe 20/5/2013, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara Basutu (Hanang) na Haydom (Mbulu).
Siku ya tarehe 21/5/2013, Katibu Mkuu wa CHADEMA atakuwa na mkutano wa hadhara Dongobesh na Mbulu Mjini. 


Tarehe 22/5/2013 akiwa njiani kuelekea Babati Vijijini, Katibu Mkuu atawasalimia wananchi wa vijiji vya Mutuka na Mwikansi kabla ya kufanya mkutano wa hadhara Galapo, Babati Vijijini, kuanzia saa 8 mchana.


Siku ya tarehe 23/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara maeneo ya Riroda, Dareda na Bashnet, Babati Vijijini.


Tarehe 24/5/2013, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Simanjiro na atafanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Musitu wa Tembo, Ngorika na Ngage.


Siku inayofuata, tarehe 25/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara katika maeneo ya Orkesimet, Namaruru kisha atamalizia kwa kufanya mkutano mkubwa Mererani, kuanzia saa 10 jioni.
Imetolewa leo, Mei 17,2013 na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...