Monday, May 20, 2013

IRINGA KUMENUKA KATIKA VURUGU ZA WAMACHINGA,MCH.MSIGWA AKAMATWA NA WENGINE 51.


Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) alikamatwa na polisi jana kwa tuhuma kuwa ndiye chanzo cha kuhamasisha wafanya biashara wadogo wadogo (wamachinga) kufanya vurugu huko Iringa.Askari polisi wa kutuliza ghasia (FFU) katika Manispaa ya mji wa Iringa pia iliwakamata zaidi ya watu hamsini, akiwemoo aliyekuwa mgombea udiwani katika kata ya Mvinjini, Abuu Majeck.

Biashara zilisimama wakati wa sekeseke hilo, moshi ulitanda kutokana na matairi kuchomwa moto katika barabara za kuu ya Iringa-Dodoma na ile ya Mashine Tatu.
Pia Mbunge huyo jana alikuwa katika eneo la chuo cha Tumaini kwenye harambee iliyokuwa imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.







No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...