Friday, May 17, 2013

KUITWA KAZINI KWA WALIOFANYA USAILI TAREHE 06-13 APRILI,2013.

                                                                 KUITWA KAZINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwaarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 06 hadi 13 Aprili, 2013 kuwa walioorodheshwa katika tangazo hili wamefaulu usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri kama ilivyoonyeshwa katika tangazo hili. Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vipya katika muda ambao umeainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
http://ajira.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_details&Itemid=0&gid=143

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...