Monday, May 13, 2013

LADY JAY DEE AFIKISHWA MAHAKAMANI NA CLOUDS FM.


MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. 
Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. ...
Mkurugenzi wa Clouds FM bwana Ruge Mutahaba.
Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu. 
Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...