Thursday, May 23, 2013

LADY JAY DEE APOTEZA NAMBA ZA SIMU ZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA LA FAMILIA 2.

 
Lady Jay Dee amekili kuwa amepoteza namba za waliochaguliwa kujiunga na La Familia 2 na kuwaomba wamtumie namba zao za simu tena ili waweze kuwasiliana kama alivyoandika katika mtandao wake wa kijamii:-

"LA FAMILLE 2

Habari ndugu zanguni.

Kwanza mtaniwia radhi, nimepoteza namba zote za simu mlizonitumia......Kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wangu. Lakini majina ya wote waliochaguliwa kujiunga na La Famille 2 ninayo.

Hivyo basi naomba mniandikie tena e-mail ya namba zenu za simu tu. Ili tufahamishane ni lini tunaweza kukutana kwa mara ya kwanza pamoja...Na kupanga mikakati ya hapo baadae.

Niko katika wakati sio mzuri sana, ki muda na mambo mengine mengine...Hivyo mtanisamahe kwa kupoteza namba zenu za simu...Kichwa kimeelemewa.

Natumaini mtanielewa
Nasubiri kusikia kutoka kwenu, soon.
E-mail ni judyjaydee@yahoo.com
Natanguliza shukrani za dhati

JayDee"

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...