Tuesday, May 21, 2013

LEO MEI 21,KUMBUKUMBU YA AJARI YA MELI YA MV.BUKOBA.

LEO ni Mei 21 siku ambayo Taifa linaingia kwenye kumbukumbu chungu ya kutimia miaka 17 tangu kutokea kwa ajari mbaya ya Mv Bukoba iliyochukua maisha ya Watanzania zaidi ya 300 waliokuwa wakisafiri kutoka Bukoba kuelekea jijini Mwanza.
Mara kadhaa watu wachache  walionusurika katika  ajari hiyo wamekuwa wakijitokeza kutoa ushuhuda wao jinsi mambo yalivyokuwa wakati  Meli hiyo ilipopinduka ikiwa inakaribia kuingia  Bandari  ya Mwanza.
Kitu cha  ajabu  ni kuwa  mpaka leo  serikali inaonekana bado iko usingizini katika  kuweka umakini  kwa vyombo vya usafiri nchini  jambo linalofanya  kuwepo kwa  ajari za  mara kwa mara  zinazogharimu maisha ya  watanzania wengi  kwa uzembe wa watu wachache.
Siku za hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia ajari mbaya za barabarani na majini ambazo zimekuwa zikiacha historia na majonzi kwenye familia mbalimbali,pia kupoteza nguvu kazi ya taifa. 
Makaburi ya pamoja ya Ndugu zetu yaliyo Igoma-Mwanza.

Hivyo ni ombi na vilio vya wananchi kwa serikali, waendeshaji vyombo vya usafiri na wadau mbalimbali wa sekta hii kuwa makini katika kudhibiti ajari zisizo za lazima kutokea....
Mwisho naomba kuwapa pole wahanga wa ajari ya MV.Bukoba na watanzania wote kwa ujumla mwenyezi Mungu awatie nguvu na kuwafariji.
Amina!!
Meli Ya MV Bukoba...ikizama Ziwa Victoria,Miaka 17 iliyopita!

Mnara wa kumbu kumbu.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...