Friday, May 10, 2013

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA - MUDA WA KUPOKEA MAOMBI WAONGEZWA.


Wizara ya afya imeongeza muda wa kupokea maombi ya nafasi za kazi hadi tarehe 20.05.2013 badala ya tarehe 10.05.2013.
Kwa taarifa zaidi za tangazo hilo la awali soma hapa chini.
                                           
                                           JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
                                         WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
                                                            TANGAZO LA KAZI
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia nafasi za kazi kwa wote wenye taaluma za Kada za Afya ambao wako tayari kufanya kazi katika Utumishi wa Umma.
Vigezo na Masharti:
1. Awe ni raia wa Tanzania.
2. Awe na umri usiozidi miaka 45.
3. Watumishi wa Kada za Afya waliojiendeleza wakiwa kazini wasitume maombi bali waombe kwa waajiri wao kubadilishwa vyeo kulingana na sifa walizopata.
4. Watumishi ambao walikwishapangiwa vituo vya kazi miaka ya nyuma na hawakuripoti au kuacha kazi hawatapangiwa vituo vya kazi, kwa sababu hawataweza kuingia kwenye ‘Payroll’ ya Serikali.
5. Maombi yote yaambatanishwe na:- Nakala ya Cheti cha Taaluma, Nakala ya Cheti cha Kidato cha nne/sita, Maelezo binafsi (CV), Picha (Passport size mbili) za hivi karibuni, Nakala ya cheti cha usajili.
6. Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha nne/sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au Wakili anayetambuliwa na Serikali.
7. Waombaji wanatakiwa kuchagua/kupendekeza maeneo matatu (Mikoa na Halmashauri) ambayo wangependa kupangiwa kazi kwa kuzingatia nafasi zilizoainishwa kwenye Kibali (Tazama Tovuti ya Wizara).
2
Waajiri wote wanatakiwa kuharakisha zoezi la kuwaajiri na kuwaingiza kwenye ‘Payroll’ ya Serikali wataalam wote watakaopangiwa vituo vya kazi kwenye mamlaka zao ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho za kujikimu kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu usio wa lazima watumishi husika.
Aidha, Waajiri wanakumbushwa kukagua na kuthibitisha uhalali wa vyeti vya kidato cha Nne na Sita vya wataalam hao kabla ya kuwaajiri.
Kwa utaratibu wa mwaka huu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hatatoa barua za kupangiwa Vituo vya kazi. Majina ya watakaopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye Tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz). Ukiona jina lako kwenye Tovuti au Gazeti nenda karipoti kwenye kituo ulichopangiwa kabla ya tarehe 25 Juni, 2013 ambako taratibu za ajira yako zitakamilishwa.
Maombi yote yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayatafanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 10 Mei, 2013.
Tangazo hili pamoja na mchanganuo wa nafasi za kazi vinapatikana katika tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz)

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...