Monday, May 6, 2013

RAIA 4 WA SAUDIA WAKAMATWA KUHUSIKA NA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA.

Polisi Mkoani Arusha inawashikilia watu 8 kwa madai ya kuhusika na mlipuko wa jana siku ya jumapili katika kanisa Katoliki la Olasit viungani mwa mji wa Arusha.
Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne (4) wa Saudi Arabia, na wengine wanne (4) ni raia wa Tanzania.
Wakati mwandishi wa BBC Baruan Muhuza akuzungumza akiwa hospitalini mjini Arusha amesema idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia mlipuko huo ni wawili na wala sio watatu kama ilivyoripotiwa hapo awali.
Polisi mjini Arusha vile vile wamethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio hilo la kigaidi ni wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza ni kilipuzi aina gani kilitumika wakati wa shambulizi hilo.
Lakini Baruan Muhuza ambaye alitembelea eneo la tukio mbali na majeruhi hakuna hasara kubwa iliyotokea mahali hapo pia sakafu na kuta za kanisa hilo hazikuchimbika sana.
Kutoka Dar es Salaam Leornad Mubali anaongezea kuwa watu wawili sana wamethibitishwa kufariki dunia katika mlipuko huo uliotokea majira ya saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha nchini Tanzania na wengine kadhaa kujeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya uzinduzi wa parokia mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi wakinusurika pia .
Kwa mjibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha mlipuko huo unapotokea walikuwa tayari katika hatua ya kubariki maji kwaajili ya uzinduzi wa kanisa ulikuwa ukiongozwa na balozi wa Papa Fransis.
Shambulizi la Arusha
Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali watu kati yao wamefariki huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru mjini Arrusha.
Shughuli zote kuhusiana na ibada hiyo zimesitishwa huku watalaalamu wa milipuko na polisi wakiendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.
Bado hakuna taarifa zozote kuhusiana na chanzo halisi cha bomu hilo ama kundi lolote linalodaiwa kuhusika na utegaji wa bomu hilo.
Hili ni shambaulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japo kuwa mwaka huu pia kulikuwa na mtukio ya mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia kanisani.
 
Chanzo:BBC

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...