Wednesday, May 8, 2013

WATU 55 WAUAWA KWA SHAMBULIZI LA BOKO HARAM

Watu waliokuwa na silaha nzito jana wamekishambulia kituo cha polisi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na kuwauwa watu 55, ikiwa ni pamoja na polisi na raia. Msemaji wa jeshi Musa Sagir amesema shambulizi hilo lilifanywa na wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu katika kituo cha polisi cha mji wa Bama, jimbo la Borno, lilisababisha vifo vya polisi 22, maafisa 14 wa gereza, wanajeshi wawili na raia wanne. Musa amesema wafuasi 13 wa kundi hilo pia walikufa katika shambulizi hilo. Kiasi ya wafuasi 200 wa kundi la Boko Haram waliokuwa na silaha nzito wanaripotiwa kuwasili wakiwa na bunduki kabla ya kuushambulia mji huo. Wapiganaji hao waliokuwa na magari aina ya pick up, kwanza waliishambulia kambi ya jeshi na kituo cha polisi kabla ya kulivamia gereza. Hakuna kundi lililotangaza rasmi kuhusika na shambulizi hilo, ijapokuwa jimbo la Borno ni ngome ya kundi la Boko Haram, ambalo maafisa wanasema ndilo lililofanya shambulizi hilo.

Source: DW

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...